Mchana wa leo nitashare nanyi namna ya kupika Rosti ya Maini. Waweza kula na wali, ugali, chapati, mikate au viazi au chochote unachopenda. Karibu
MAHITAJI
Maini ya ng'ombe
Kitunguu swaumu kilichosagwa
Tangawizi iliyosagwa
Kitunguu maji 1
Chumvi
Mafuta ya kupikia
Pilipili kichaa 1
Biringanya 1
Pilipili hoho 1
Karoti 1
Viazi mviringo 2
Nyanya 2
Tui la nazi
Kitunguu swaumu kilichosagwa
Tangawizi iliyosagwa
Kitunguu maji 1
Chumvi
Mafuta ya kupikia
Pilipili kichaa 1
Biringanya 1
Pilipili hoho 1
Karoti 1
Viazi mviringo 2
Nyanya 2
Tui la nazi
JINSI YA KUPIKA
-Katakata maini katika vipande vidogo na kisha vioshe
-Chuja maji na uweke kwenye sufuria
-Weka sufuria kwenye jiko, washa moto na ongeza chumvi na mchanganyiko wa kitunguu swaumu na tangawizi zilizosagwa
-Acha maini yachemke, ongeza maji moto pale yanapokaukia mpaka yaive kabisa
-Epua maini yako tayari kwa kuyaunga
-Chukua sufuria safi, weka kwenye moto
-Ongeza mafuta na acha yachemke kiasi kisha ongeza chumvi
-Ongeza vitunguu maji na vipike mpaka vibadilike rangi
-Ongeza mchanganyiko wa vitunguu swaumu na tangawizi vilivyosagwa
-Ongeza pilipili hoho na biringanya na koroga taratibu na viache viive
-Chukua karoti iliyokatwakatwa na viazi mviringo ambavyo utakua umevichemsha kidogo viongezee kwenye sufuria yako
-Ongeza maini yaliyochemka, pamoja na viungo unavyopendelea
-Ongeza nyanya na uache iivie huko ili kutengeneza rojo
-Ongeza tui la nazi na koroga bila kuacha mpaka unapoona mboga inataka kuchemka, ila hakikisha tui halikatiki kwa kuchemka
-Epua mboga yako tayari kwa kuliwa.
No comments:
Post a Comment